10 kubwa kuhusu Rashid Mfaume Kawawa (May 27, 1926 – December 31, 2009)

HomeElimu

10 kubwa kuhusu Rashid Mfaume Kawawa (May 27, 1926 – December 31, 2009)

 

1. Kawawa alikutana na Nyerere wakiwa wanafunzi Shule ya Tabora Boys.

2. Kawawa alimgomea baba yake mzazi kuendelea na masomo Chuo Kikuu cha Makerere Uganda, na kumshauri Baba yake hiyo pesa asomeshee wadogo zake.

3. Alikuwa Waziri Mkuu mara mbili, Waziri Mkuu Tanganyika 1962 baada ya Nyerere kujiuzulu, akawa tena Waziri Mkuu wa Tanzania 1972 – 1977.

4. Kawawa alishawahi kuwa Waziri wa Ulinzi 1977 – 1980.

5. Wakati Nyerere anang’atuka madarakani 1985, majina matatu yalipendekezwa kugombea, Kawawa, Ally Hassan Mwinyi na Salim Ahmed Salim mmoja apitishwe kugombea urais wa Tanzania. Kawawa aliomba kutolewa kwenye mchakato wa kinyang’anyiro kwani amefanya kazi muda mrefu sana na Mwalimu kwa hiyo angetamani awapishe watu wengine kwenye nafasi za uongozi. Mpambano ukabakia kati ya Ally Hassan Mwinyi na Salim Ahmed Salim, Mwinyi akapitishwa kugombea akawa Rais.

6. 1964 Kawawa alikuwa Makamu wa Rais wa Pili wa Tanzania baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

7. Kawawa ana shahada mbili ya heshima kutoka Chuo Kikuu cha Makerere Uganda na Chuo Kikuu cha Dodoma ambazo zote alizipewa wakati ameshafariki.

8. Kawawa alikuwa mnazi mkubwa wa sera za kijamaa kwenye kuendesha uchumi, haishangazi kuona waliiva sana na Mwalimu.

9. Tarehe 27 February 2017 Serikali ilifungua makumbusho maalumu wilayani Songea kumuenzi. Makumbusho hayo yapo Mtaa wa Kawawa, Bombambili Songea Mkoani Ruvuma.

10. Ukiacha siasa, Kawawa anashikilia rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuwa msimamizi wa kuandaa filamu (Director), mwaka 1951 alisimamia filamu ilyoitwa ‘Muhogo Mchungu’, pia alikuwa mwandika mswada ya filamu (scriptwritter).

error: Content is protected !!