Breaking: Mfahamu mtu wa pili kupona virusi vya UKIMWI duniani

HomeKimataifa

Breaking: Mfahamu mtu wa pili kupona virusi vya UKIMWI duniani

Mwanamke mmoja kutoka Taifa la Argentina amekuwa mtu wa pili duniani kuingizwa kwenye kumbukumbu ya watu waliopona virusi vya UKIMWI bila kutumia dawa yeyote ile.
Chembe hai (cells) zaidi ya bilioni 1 kutoka kwenye mwili wa mwanamke huyo na kuchunguzwa na kugundulika kuwa hana maambukizi tena.

Mwanamke huyo kutoka Argentina amekutwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI Machi 2013, miaka nane baadae amepimwa tena mara 10 kujiridhisa lakini bila kukuta hakukutwa na kirusi hata kimoja kwenye mwili wake.

Mwanamke huyo mara nyingine hakuwa mwenye kutumia dawa za ARV kupunguza kasi ya virusi. Majibu yake yameshangaza wanasayansi na kusema kuwa huenda  anakinga mwili ambayo ni adimu sana kwa watu wengine na yenye uwezo wa kuzuia virusi kuendelea kuzaliana.

> Madiwani wataka Kondomu ziongezwe

“Kilichotokea ni cha kipekee sana”, amesema Dk. Steven Deeks mtafiti wa masuala ya virusi vya UKIMWI kutoka Chuo Kikuu cha California San Francisco. “Sio kwamba anaweza kuvidhibiti virusi, lakini yeye hana kirusi hata kimoja, hii inashangaza sana”. Ameendelea kusema.

Andiko juu ya mwanamke huyo limechapishwa siku ya jumatatu 15 Novemba 2021 kwenye jarida la ‘Annals of Internal Medicine Journal’. Virusi vya UKIMWI hadi hivi leo bado havina tiba, lakini wapo watu watatu wamepona virusi hivyo baada kuingiziwa seli maalumu kwa ajili ya matibabu ya saratani. Kesi ya Mwanamke huyo wa Argentina ni tofauti kabisa kwani hakuwa ametumia dawa yeyote.

Bado watafiti wanakesha kutafuta dawa ya virusi vya Ukimwi, hadi hivi sasa watu wa aina hiyo wako wawili tu ambao chembe hai zao zina uwezo wa kupambana na virusi vya UKIMWI bila kutumia dawa yeyote. Dr. Deeks anasema kuwa kama watafanikiwa kuelewa namna miili ya wanawake hao inavyofanya kazi, basi tutakuwa na uwezo wa kutengeneza dawa za kuponesha UKIMWI.

 

error: Content is protected !!