Jeshi la Umoja wa Ulaya (EU) lawafuata magaidi Msumbiji

HomeKimataifa

Jeshi la Umoja wa Ulaya (EU) lawafuata magaidi Msumbiji

Wakati vita dhidi ya magaidi ikipamba moto nchini Msumbiji katika eneo la Cabo Delgado, Umoja wa Ulaya umeazimia kujiunga na SADC pamoja na Rwanda kupambana na ugaidi. Umoja wa Ulaya kuingia katika vita dhidi ya ugaidi nchini Msumbiji itasaidia sana kuimarisha usalama nchini humo.

Akizungumza na vyombo ya habari Septemba 14 Jenerali Nuno Lemos Pires alisema kuwa misheni dhidi ya ugaidi Cabo Delgado katika maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji mpakani na Tanzania itaanza rasmi mwishoni mwa mwaka 2021. Alisema pia kuwa kuna kuna 10 – 12 kutoka Umoja wa Ulaya ambazo zitashiriki katika mapambano hayo, na pia zipo nchi nyingine kutoka nje ya umoja wa Ulaya zimeshajitolea kutoa msaada.

Umoja wa Ulaya unatarajia kupeleka wanajeshi 120 ambao watatoa mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji ikiwamo wanajeshi wa majini na makomando. Majeshi ya Umoja wa Ulaya yatakuja Msumbiji baada ya Umoja wa nchi za SADC (SAMIM) pamoja na majeshi ya Rwanda kuenda Msumbiji kutoka msaada.

Watu zaidi ya 700,000 wamehama makazi yao kutokana na vita hiyo. SADC imepeleka wanajeshi 700 huku Rwanda ikitoa wanajeshi 1000 ambao wamekweta baada ya makubaliano baina baina nchi hizo mbili.

error: Content is protected !!