Harmonize, Diamond watofautiana

HomeBurudani

Harmonize, Diamond watofautiana

Msanii na mmiliki wa lebo ya Konde Gang, Rajabu Abdul maarufu kama Harmonize ametofautiana kimawazo na aliyewahi kuwa msimamizi wake kutoka lebo ya Wasafi, Diamond Platnumz katika ushindi wa tuzo za nyumbani na nje.

Hivi karibuni limefanyika tukio la ugawaji wa Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) na Diamond alinukuriwa akisema kwamba kwa sasa haitaji tuzo za nyumbani bali anataka za kimataifa kama BET na Grammy’s huku akisema anaona kwa kufanya hivyo ataleta ushindani kimataifa na kukuza muziki wa bongo fleva.

Jana Aprili 5, 2022 Harmonize aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba yeye haziwazi wala kutamani kushinda tuzo za Grammy’s na BET bali anataka kuhakikisha anachukua tuzo za nyumbani kama ambavyo ameshinda tuzo 3 za muziki Tanzania mwaka huu.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by KONDEBOY (@harmonize_tz)

Pia , Harmonize aliandika kwamba haitaji kushinda tuzo za Grammy’s na BET kama atashindwa kupata tuzo za ndani na kukiri kwamba TMA 2022 lazima atachukua zingine.

error: Content is protected !!