Takukuru yamkalia kooni Raibu

HomeKitaifa

Takukuru yamkalia kooni Raibu

Taasisi ya Kupigana na Kupambana na Rushwa, (Takukuru) imesema imepokea malalamiko yamhusiyo aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi Mjini, Juma Raibu na wanaendelea na uchunguzi.

Aprili 11 Raibu alivuliwa madaraka kufuatia kura zilizopigwa na baraza la madiwani nyingi zikimpinga. hii ilitokana na Raibu kuhudhuria sherehe ya mashoga jambo ambalo halikuafikiwa na jamii na viongozi wenzake.

Frida Wikes, Kamanda wa Takukuru, Kilimanjaro ameiambia Mwananchi kuwa amepokea taarifa na tuhuma za rushwa zinazomhusu Raibu.

raibu aliwahi kukutwa katikati ya sakata la kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Sabaya kumdhulumu mfanyabiashara Elioth Lyimo shilingi milioni 25.

error: Content is protected !!