Rais Samia kuhudhuria Uzinduzi wa ‘Tanzania Royal Tour’

HomeElimu

Rais Samia kuhudhuria Uzinduzi wa ‘Tanzania Royal Tour’

Baada ya kushirika katika uandaaji wa filamu ya kutangaza utalii wa ndani maarufu kama ‘Tanzania Royal Tour’ iliyoandaliwa na Mtozi kutona Marekani, Peter Greeberg, ‘starring’ wa filamu hiyo, Rais Samia anatarajiwa kuwepo kwenye uzinduzi wa filamu hiyo nchini Marekani Aprili 18, 2022.

Rais Samia kama mwenyeji wa wageni hao alifanikiwa kuwatembeza katika vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa inayoongoza Afrika (Africa’s Leading National Park), Serengeti pamoja na kuwaonesha upekee na utajiri wa Tanzania kuanzia madini ya Tanzanite na mandhari yenye kuvutia.

Awali, filamu hiyo iliyotarajiwa kurushwa hewani kupitia vituo mbalimbali vya runinga vya Tanzania Aprili 21, 2022 hatimaye itawahi siku mbili kabla.

Rais Samia ameondoka nchini usiku wa kuamkia jumanne kuelekea Marekani kwa shughuli za kiofisi. Pamoja na hayo atashiriki pia kwenye uzinduzi wa filamu hiyo yenye lengo la kuitangaza Tanzania na shughuli zake za utalii, uchumi, uwekezaji, utamaduni na mambo mengi yaihusuyo nchi hii.

 

error: Content is protected !!