JJ Mungai wafurahia madarasa ya Samia

HomeKitaifa

JJ Mungai wafurahia madarasa ya Samia

Walimu, wazazi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari JJ Mungai iliyopo halmashauri ya Mjini wa Mafinga wameeleza furaha yao kwa ujenzi wa madarasa uliofanyika katika kipindi cha muda mfupi tofauti na awamu za nyuma ambapo ingechukua muda mrefu kukamiliza kwa mradi huo.

Kelvini Tindi ni mmoja wa wanafunzi ambaye amesema siku ya kwanza kufika kwenye madarasa hayo na hali aliyokutana nayo.

“Kwanza siku ya kwanza kuingia katika hili darasa nilijisikia vizuri kwa sababu miundo mbinu ilivyoboreshwa,” alisema Kelvini.

Mwamsumbi Peter ni mzazi wa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, naye anaelezea furaha yake na pongezi kwa serikali ya awamu ya sita kwakuweza kukamilisha ujenzi wa madarasa ndani ya muda mfupi.

“Viti vimekuwepo, watoto wanafuraha kwahiyo yamekuwa madarasa ya mfano alafu kinachonishangaza ni kwamba ni muda mfupi kumbe mambo yanawezekana .Ni kipindi cha mwaka mmoja toka yaanze kufanyika haya ndio maana inanishangaza , huu ni usimamizi mzuri wa serikali yetu,” alisema Bwana Peter. 

error: Content is protected !!