Uzalishaji Umeme na gesi asilia waongezeka nchini

HomeKitaifa

Uzalishaji Umeme na gesi asilia waongezeka nchini

Wizara ya Nishati imesema uwezo wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyoungwa katika mfumo wa gridi ya taifa umeongezeka na kufi kia megawati 1,777.05 Desemba mwaka jana.

Waziri January Makamba amesema jijini Dodoma ongezeko hilo ni sawa na asilimia 4.87 ikilinganishwa na megawati 1,694.55 zilizokuwapo hadi kufikia Septemba mwaka jana.

Makamba alisema hayo wakati Wizara ya Nishati ilipowasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati taarifa ya Wizara kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana. Amesema katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana, futi za ujazo milioni 38,172 za gesi asilia zilizalishwa katika vitalu vya Songosongo na Mnazi Bay.

Makamba amesema uzalishaji wa gesi asilia umeongezeka kwa asilimia 27 ikilinganishwa na kipindi cha Julai-Desemba mwaka 2021 wakati zilipozalishwa futi za ujazo 29,996.

“Ongezeko hili limetokana na ufungaji wa kompresa tatu katika Kitalu cha Songosongo ambazo zimeongeza mgandamizo na msukumo wa gesi kutoka kisimani na sasa wastani wa futi za ujazo milioni 240 zinazalishwa kwa siku kutoka katika vitalu vya Songosongo na Mnazi Bay,” amesema Makamba.

error: Content is protected !!