Rais wa Burundi ajitwika msalaba

HomeKimataifa

Rais wa Burundi ajitwika msalaba

Ijumaa Kuu ni siku ya kukumbuka mateso ya Yesu na makanisa mbalimbali kuigiza mateso ya Yesu kama njia ya kufundisha waumini kuhusu alivyojitoa Yesu kwa wanadamu, Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi ameonekana katika picha akiwa amejitwika msalaba hapo jana.

Yesu  kubeba msalaba kama ishara ya dhambi na mateso ya wanadamu, baadhi ya wananchi wa Burundi wamezungumza mitandaoni na kuuliza Je! Rais wao alikuwa na maana gani?

Wengine wameishia kusema ni aibu kufanya kitendo hicho lakini pia wengine kusema angeweza kutumia msalaba mzuri zaidi kwani aliotumia si mzuri na ni dhahiri kuwa amekata mti ili kutengeneza msalaba huo.

Aliyepost picha hiyo alisema “Huu ungeitwa unyenyekevu na kufanya Rais aheshimiwe. Je, Burundi hakuna uwezo wa kutumia msalaba mzuri zaidi ya miti iliyokatwa msituni kwangu na sasa ameubeba rais?”

Haya ni baadhi ya maoni ya watu kuhusu picha hiyo ambayo pia yanaweza kutafsiriwa kwa lugha ya kiingereza;

error: Content is protected !!