Bodaboda ajinyonga kwa mkanda

HomeKitaifa

Bodaboda ajinyonga kwa mkanda

Idrisa Salum Milundiko (24), mkazi wa Kitongoji cha Kasokola Mashariki B wilayani Mpanda, Mkoa wa Katavi anayejihusisha na uendeshaji wa bodaboda, amekutwa amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali chanzo kikiwa ni msongo wa mawazo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ali Makame Hamad ameeleza kuwa Aprili 8, mwaka huu Milundiko alitoweka nyumbani kwao na kuacha ujumbe mfupi wa maandishi uliokuwa ukisema “Kaka mimi naenda kujinyonga kwani nina matatizo mengi na mwili wangu upelekwe kwa mjomba wangu aishie Makanyigio,” alinukuu Kamanda Hamad.

Alieleza kuwa baada ya hapo kijan ahuyo hakuonekana tena hadi alipokutwa akiwa amejinyonga porini majira ya saa sabab na nusu mchana Aprili 13, mwaka huu.

Kamanda Hamad alieleza polisi ilibaini chanzo cha dereva huyo wa bodaboda kujinyonga ni msongo wa mawazo, hivyo mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya kuendelea na utaratibu za mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi.

 

error: Content is protected !!