Mwizi azawadiwa pesa na kazi

HomeKimataifa

Mwizi azawadiwa pesa na kazi

Kijana mmoja aliyefungwa kwa wizi wa vyakula na kupigwa faini ya takribani milioni 2 aachiwa huru na marupurupu.

Aliyekuwa gavana wa Kenya, Mike Sonko amemlipia faini yote kijana Alvin Chivondo (22) na kumpatia chakula cha kutosheleza mwezi mzima kufuatia kijana huyo kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.

Kijana huyo aliiba kilo tano za mchele, majani ya chai, sukari kilo mbili, mafuta ya kupikia lita tano na asali vyenye thamani ya Ksh. 3,165 sawa na Tsh 63078.23 na kupigwa faini ya Ksh 100,000 sawa na Tsh 1992993.03.

“Nimefurahi kijana huyo sasa yuko huru. Ni matumaini yangu atakuwa mtu wa kuwajibika. Manunuzi yalifanyika kwenye supermarket hiyo hiyo ambapo alikamatwa baada ya kuiba vyakula kwaajili ya kuilisha familia yake,” amesema Sonko.

Mbali na chakula, Chivondo pia alipewa njia ya kujipatia kipato.

“Tumempa Alvin Chivondo kazi katika ofisi zetu za Upper Hill na timu yetu imemuonyesha kazi yake inahusu nini,” aliongeza Sonko.

Mbali na kulia na kuomba msamaha mahakamani, hakimu alishindwa kumsamehe Chivondo kwani hii haikuwa mara yake ya kwanza kufanya tukio hilo, kwani Aprili 3 katika supermarket hiyohiyo alikamatwa tena na kupelekwa kituo cha polisi ambao walimsamehe na kumwacha huru.

error: Content is protected !!