Alichosema Harmonize msibani kwa Maunda Zorro

HomeBurudani

Alichosema Harmonize msibani kwa Maunda Zorro

Ikiwa leo Aprili 16,2022 mwili wa msanii wa bongo fleva Maunda Zorro, umepumzishwa kwenye makazi yake ya milele ambapo watu wengi wakiwemo wasanii walijitokeza kuungana na familia ya Mzee Zorro katika maziko ya binti yake, msanii Harmonize alichaguliwa kwenda kuweka ua kwa niaba ya wasanii wenzake.

Akitoa salamu za pole kwa familia, Harmonize aliwataka wasanii wenzake wajitathmini maisha yao pamoja na kuendelea kuwa karibu na familia ya marehemu kwani ameacha watoto wadogo watatu.

“Kifo kinazunguka na wewe muda wote na ni wakati wa kujiandaa, unajua tunaishi katika dunia ambayo ina vitu vingi na vishawishi vingi ukizingatia hapa sisi wengi ni vijana lakini tunapopata muda wa kumshukuru Mungu na tuishi na watu vizuri kwa sababu gani huwezi jua kesho nani atakuja kukustili,” alisema Harmonize.

Aidha, Harmonize ameiomba Serikali kuitazama familia ya mzee Zorro kwani imekuwa na mchango mkubwa sana katika ukuaji wa tasnia ya muziki ikizingatiwa watoto wake wawili, Marehemu Maunda Zorro na Banana Zorro ni wanamuziki wa muda mrefu sana.

Maunda Zorro ameacha watoto watatu wakiume na mchumba ambaye walikuwa mbioni kufunga ndoa.

error: Content is protected !!