Musukuma ajiuzulu

HomeKitaifa

Musukuma ajiuzulu

Mbunge wa Geita Vijijini ambaye pia ni Balozi wa Mazingira anayewakilisha Bunge, Joseph Kasheku (Musukuma) amejiuzulu ubalozi wa mazingira kufuatia ripoti mbovu iliyowasilishwa kwa wabunge kuhusu kuchafuka kwa Mto Mara.

Tume iliyoundwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo imewasilishwa na Profesa Manyele kwa wabunge ripoti ya uchunguzi wa chanzo cha kuchafuka kwa maji ya Mto Mara na kusababisha vifo vya samaki, ripoti iliyokataliwa na wabunge wote 18 wanaounda kamati hiyo wakisema majibu ya ripoti hiyo ni ya aibu na isichapwe mtandaoni.

Kutokana na aibu hiyo Musukuma aliamua kujiuzulu.

“Mimi nilikuwa Balozi wa Mazingira ninayewakilisha wabunge ambaye nilichaguliwa na Waziri Jafo (Dkt. Jafo), natangaza kuanzia leo kuwa nimejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo maana hii ni aibu sana,” amesema Musukuma.

Ameongeza kuwa yeye haikubali ripoti hiyo na tume mpya iundwe kwenda kufanya kazi hiyo.

error: Content is protected !!