Mkurugenzi Mange App kizimbani

HomeKitaifa

Mkurugenzi Mange App kizimbani

Mkurugenzi wa Mtandao wa Kijamii wa U turn Collection, Allen Mhina (31) na wenzake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka matatu yakiwemo ya kuchapisha maudhui yanayokiuka haki na uhuru wa mtu mwingine na kumfedhesha mtu kwa njia ya mtandao (cyber Bullying).

Mbali na Mhina, ambaye ni mkazi wa Temeke, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya jinai namba 57/2022 ni Mtandao wa U turn Collection na Mange Kimambi App.

Mhina na wenzake wamesomewa mashtaka yao, Ijumaa ya wiki iliyopita mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.

error: Content is protected !!