Tatizo la afya ya akili limekua likiongezeka kwa kasi hususani kwa vijana, Watu wachache hugundua kuwa wana matatizo ya afya ya akili lakini kwa sehemu kubwa ngono inaweza kupunguza tatizo hilo kama ifuatavyo;
1. Ngono inapunguza msongo wa mawazo
Afya ya akili kwa kiasi kikubwa huathiriwa na msongo wa mawazo, msongo wa mawazo unatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine kutokana na mitazamo mfano kuna watu kuolewa kwao ni kipaumbele hivyo ikitokea wamechelewa kuolewa wanakua na msongo wa mawazo kwa kiasi kikubwa.
Miongoni mwa dalili za msongo wa mawazo ni kama maumivu makali ya kichwa, kukosa usingizi pamoja na kupungua kwa kinga ya mwili, Unaposhiriki ngono na mwenzio na kufika kileleni ubongo unatoa kemikali mbalimbali ikiwemo homoni ya Polactin ambayo inapunguza msongo na kukufanya ulale usingizi mzuri.
Utafiti unaonyesha kuwa kufanya mapenzi mara kwa mara hupunguza shinikizo la damu linalohusiana na msongo wa mawazo.
2. Ngono huongeza kujiamini
Kufanya ngono mara kwa mara kunasiadia mwili kutoa homoni ya Oestrogen, homoni hii inasaidia kufanya mwili uonekane mdogo zaidi yaan wa ujana utafuti unaonyesha kuna uhusiano kati ya kufanya ngono mara kwa mara pamoja na kuonekana kijana nao ni watu wanaofanya ngono sana hawaoni aibu kuelezea maisha yao ya ngono kwani matokeo yake ni chanya katika mionekano yao.
3. Ngono inaongeza ukaribu
Ngono inakufanya uwe karibu na mwenzi wako, Matamanio ya kingono hutofautiana hivyo mnapofanikiwa kila mmoja kutimiza matamanio ya mwenzie mnatengeneza muunganiko imara wa pamoja ambao utakufanya uwe huru na uwe na uwezo wa kuongea chochote mbele ya mwenzi wako unapokua na tatizo.