Serikali yaweka neno matukio ya mauaji

HomeKitaifa

Serikali yaweka neno matukio ya mauaji

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum chini ya waziri Dk. Doroth Gwajima, imezitaka kamati za kupinga ukatili kwenye maeneo mbalimbali nchini kutekeleza majukumu yake ipasavyo na  jamii kushiriki kukabili matukio hayo yaliyoshika kasi.

Dk. Gwajima aliyasema hayo jana bungeni akijibu swali la mbunge wa Iringa Mjini (CCM), Jesca Msambatavango, aliyetaka kujua moja ya changamoto anayoanza nayo (Waziri) kwenye wizara hiyo ni mauaji yanayoendelea kwenye jamii yanayotokana na jinsia ikiwamo mume kuua mke, mke kuua mume na mtoto kuua mzazi kwa sababu ya mali.

“Tunao mkakati wa kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto, mpango wa taifa uliozinduliwa mwaka 2017/2018 unakwenda mpaka 2021/2022. Umeandaa kamati kwenye vijiji vinavyoongozwa na wenyeviti wa serikali za vijiji, mtaa, kata, halmashauri mpaka taifa na mkoa ukiwamo,” alisema Dk. Gwajima.

Pamoja na hayo waziri Gwajima aliongezea kuwa iwapo kamati hizo zitatekeleza majukumu yake yaliyomo kwenye mwongozo itaweza kudhibiti ukatili unaotokea kwenye jamii kwa kuona viashiria husika na kuvitolea taarifa vyombo vya dola.

error: Content is protected !!