Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema mfumo mpya wa usahihishaji mitihani utaokoa shilingi milioni 550 zinazotengwa kwa ajili ya kusimamia zoezi hilo na pia litaondoa suala la kusahihisha kwa upendeleo kwani msahihishaji hatoweza kujua jina la mwanafunzi, namba ya mtihani na hata jina la shule.
“Mafanikio mengine ya elimu ni kuwa mfumo mpya wa usahihishaji umetengenezwa unaongeza umakini na unaondoa upendeleo na rushwa ni mfumo wa kwanza barani Afrika, ukianza kutumika utaokoa shilingi milioni 550 zinazotumika kugharamia ushahihishaji mitihani,” alisema Profesa Mkenda.
Akieleza namna mfumo huo utakavyokuwa unafanya kazi , Profesa Mkenda kuwa mitihani itakua ikisahihishwa na wlaimu wakiwa kwenye shule zao lakini kupitia mfumo mpya wa kieletroniki ambapo watatakiwa kujaza taarifa zao na kuona swali moja wanalotakiwa kusahihisha.
Pia alisema, kila mwalimu atakuwa anafanyia kazi swali moja tu litakalotokea pindi ajazapo taarifa zake na kumalizia kwamba mfumo huo upo kwenye hatua mwisho za majaribio na pindi ukikamilika utaweza kuokoa shilingi milioni 550.