Ahadi ya Makamba yatimia Kigoma

HomeKitaifa

Ahadi ya Makamba yatimia Kigoma

Itakumbukwa wakati akiwasilisha Bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati Juni 2,mwaka 2022, Waziri wa Nishati, January Makamba alikitaja kipaumbele cha kwanza kuwa ni, “Kutekeleza miradi mbalimbali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme, ikiwemo kupeleka umeme wa Gridi ya Taifa kwenye mikoa ya Katavi, Kigoma na Kagera na mradi mkuwa wa kuimarisha Gridi ya Taifa (National Grid Stabilization Project).

Julai, mwaka 2022, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi pale Nyakanazi, Waziri Makamba aliwaahidi wananchi wa Nyakanazi kuwa ifikapo Oktoba, mwaka huu watakuwa wanapata umeme kutoka kwenye Gridi ya Taifa. Ahadi hii imetimia kabla hata ya mwezi Oktoba 2022 kufika.

Hivi sasa, serikali inaenda kuokoa zaidi ya bilioni 22 zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa ajili ya kuendesha majenereta ya mafuta yaliyokuwa yakitoa huduma kwa wananchi.

Faida ya Kigoma kuingizwa Gridi ya Taifa

– Kuimarika kwa upatikanaji wa umeme kwenye maeneo yaliyokuwa yanategema umeme uliokuwa ukizalishwa na majenereta ya mafuta.
– TANESCO inaokoa jumla ya shilingi bilioni 22.4 kwa mwaka kwa kuzima mitambo wilaya ya Kibondo na milioni 734 gharama ya matengenezo na bilioni 8.7 gharama ya kunua mafuta ya dizeli.

– Kwa wilaya ya Kasulu, TANESCO inakwenda kuokoa Sh1.1 bilioni kwa mwaka ambazo ni gharama za matengenezo ya mitambo na Sh11.85 bilioni kwa mwaka zikiwa ni gharama za kununua mafuta ya dizeli.

 

 

error: Content is protected !!