Aliyetupa kichanga pipa la taka auliwa

HomeKimataifa

Aliyetupa kichanga pipa la taka auliwa

Mwanamke mmoja raia wa Marekani ameuliwa na mpenzi wake ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu mwanamke huyo atupe mwili wa mtoto wao kwenye pipa la taka.

Carl Jones (44) yupo mikononi mwa polisi tangu Alhamis kwa kumchoma kisu hadi kufa mpenzi wake, Ladonia Boggs (39) usiku wa manane.

Mei 5, 2021 Boggs alimwambia mpenzi wake kuwa mtoto wao mwenye miezi miwili alichukuliwa na watu wa ustawi wa jamii na hatarudi muda wowote, lakini mpenzi wake alifuatilia na hakupata jibu.

Siku kadhaa mbele mwanamama huyo alijisalimisha polisi na kukiri kuutupa mwili wa mtoto wake kwenye pipa la takataka baada ya kujawa na hofu alipomwona amefariki.

Kuhusu kifo cha mtoto huyo, mwanamama huyo amebadili badili hadithi lakini moja anadai kuwa alitumia dawa na kisha kujikuta amemlalia mtoto na hapumui tena huku pia akisema alimbana mtoto ukutani bila kukusudia na alipoamka tayari mtoto huyo alishapoteza maisha.

Kesi zote mbili bado zinaendelea kufanyiwa uchunguzi

error: Content is protected !!