Waziri wa Maji Mhe Juma Aweso atinga katika ofisi za DAWASA usiku wa kuamkia Novemba 18, 2021, Waziri alizuru katika ofisi hizo jijini Dar es Salaam ili kuweka msisitizo kwenye mambo mabalimbali kwenye kipindi hiki ambacho Dar es Salaam inakabiliwa na changamoto kubwa ya maji katika maeneo mengi.
Baada ya kufika katika Ofisi hizo alisisitiza uwepo wa mgao sawa wa maji katika maeneo yote kusiwepo na upendeleo, lakini pia aliendesha kikao na watendaji usiku kucha kuhusu suluhu ya muda mfupi na muda mrefu pamoja na kuwapa hamasa watumishi katika kipindi hiki kigumu.
Katika kikao hiko, Mhe. Juma Aweso amewataka watumishi kutumia taaluma yao pamoja na ubunifu kusaidia wakazi wa Dar es Salaam kukabiliana na changamoto iliopo lakini pia amesisitiza watumishi wa Mamlaka kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha maji yanatoka kulingana na ratiba.
> Kauli ya Rais Samia kuhusu mgao wa maji
Pamoja na hayo ametaka DAWASA kutoa bei elekezi kwa watoa huduma binafsi wa maji kupitia magari (Bowsers), Sambamba na miongozo iliyotolewa Mhe Juma Aweso alihaidi kupitia wizara yake ya Maji watatoa ushirikiano kwa wafanyakazi hao kukabiliana na changamoto za Bonde la Wami na Ruvu.
Ikumbukwe katika muda wa kipindi cha hivi karibuni tatizo la maji Jijini Dar es Salaam limekua likilalamikiwa sana, DAWASA iliamua kutoa ratiba ya mgao wa maji kwa maeneo ya Dar es Salaam lakini pia Mhe Waziri Kassim Majaliwa alienda kutembelea mradi wa maji Ruvu.