Baba Mtakatifu Francisko afariki dunia akiwa na miaka 88

HomeKimataifa

Baba Mtakatifu Francisko afariki dunia akiwa na miaka 88

Vatican – Katika siku ya Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, Baba Mtakatifu Francisko amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 88. Alifariki akiwa katika makazi yake ya Casa Santa Marta, ndani ya jiji la Vatican.

Taarifa rasmi ya kifo chake imetolewa na Mwadhama Kardinali Kevin Farrell, aliyesema kwa huzuni kubwa:

“Ndugu wapendwa, kwa masikitiko makubwa na moyo mzito, natangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko. Tumempoteza kiongozi wa kiroho aliyejitoa kwa dhati katika huduma kwa Kanisa na kwa binadamu wote.”

Baba Mtakatifu Francisko atakumbukwa kwa moyo wake wa unyenyekevu, upendo kwa maskini, na juhudi zake za kudumisha haki, amani na mshikamano duniani.

error: Content is protected !!