Bandari ya Kilwa yaanza kupokea meli za shehena ya bidhaa mchanganyiko

HomeKitaifa

Bandari ya Kilwa yaanza kupokea meli za shehena ya bidhaa mchanganyiko

Bandari ya Kilwa imeendelea kufungua milango mipya ya kibiashara baada ya kuanza kupokea Meli za shehena ya bidhaa mchanganyiko kwenda Nchini Comoro.

Bandari hiyo ambayo ipo chini ya Bandari ya Mtwara imepokea Meli ya MV. CAPTAIN NAS – 2 ambayo imewasili tarehe 4 Disemba, 2025 katika Bandari hiyo kutokea Nchini Comoro kwa lengo la kupakia takribani Tani 700 za shehena ya mbao, vyakula na vinywaji ambavyo vinasafirishwa kwenda katika Nchi hiyo.

Akizungumzia mafanikio hayo, Meneja wa Bandari ya Mtwara Bw. Ferdinand Nyathi ameeleza kuwa mbali na kupokea Meli za Utalii, Bandari hiyo inatarajiwa kuendelea kupokea wastani wa Meli 3 kwa mwezi ambazo zitakuwa zinawasili kupakia shehena za bidhaa mchanganyiko kwenda Nchini Comoro. Bw. Nyathi ameeleza kuwa hiyo ni hatua kubwa katika kuongeza mapato na kukuza uchumi wa Mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

error: Content is protected !!