Ingawa bei za mafuta zimeendelea kupanda hapa nchini, matumaini ya kushuka kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia yameanza kuonekana.
Taariffa ya mtandao wa Trending Economics ilionyesha hadi Julai 06,2022 bei ya mafuta ghafi kwa pipa ilikuwa Dola 101.4 (sawa na Sh233,220) ukilinganisha Dola 115.4 (sawa na Sh265,420) mwezi uliopita.
Kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo kwenye soko la dunia kunaashiria uwezekano wa kupungua kwa bei miezi miwili ijayo kwa mujibu wa Katibu wa Taasisi ya Wafanyabiashara wa Mafuta ya Rejareja Tanzania (Tapsoa), Augustino Mmasi.
“Mafuta tunayotumia sasa yalinunuliwa miezi miwili iliyopita kati ya Aprili na Mei, hivyo tutanunua sasa na mchakato wa kuyaleta ni baada ya miezi miwili,”alifafanua Mmasi.