Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema ni faraja kubwa kuona boti ya utafutaji na uokoaji imeshushwa katika maji kuanza kazi katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza.
Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 unaolenga kuimarisha usalama wa watumiaji wa ziwa hilo ambalo ni muhimu kwa uchumi na maisha ya wananchi.
Rais Dk. Samia alieleza hayo jana kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii na kufafanua takriban wananchi milioni sita wanajishughulisha na uvuvi na wanahitaji nyenzo hizo muhimu kwa usalama wao.
“Mpango wa serikali ni kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya uokozi na huduma za dharura majini, ili kuhakikisha kila mwananchi anakuwa salama anapokuwa kazini au safarini.” aliandika Rais Dkt. Samia.
Ni faraja kubwa kuona Boti ya Utafutaji na Uokoaji imeshushwa kwenye maji ili kuanza kazi katika Ziwa Victoria mkoani Mwanza, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM (2020-2025) unaolenga kuimarisha usalama wa watumiaji wa ziwa hilo ambalo ni muhimu kwa uchumi na maisha ya wananchi.… pic.twitter.com/yionQesh7M
— Samia Suluhu (@SuluhuSamia) July 7, 2025