Chanzo cha kukatika umeme Mbagala

HomeKitaifa

Chanzo cha kukatika umeme Mbagala

Wizara ya Nishati, imetaja chanzo cha kukatika umeme jimbo la Mbagala, Dar es Salaam, kuwa ni kuzidiwa kwa Kituo cha Kupoza Umeme cha Mbagala.

Imesema kutokana na hali hiyo, serikali kupitia Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) imefunga transfoma yenye uwezo wa MVA 120 kutatua changamoto hiyo.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Judith Kapinga, alisema hayo bungeni, jijini Dodoma jana alipojibu swali la Abdallah Chaurembo (Mbagala0 CCM).

Mbuge huyo alitaka kujua lini tatizo la kukatika umeme mara kwa mara katika kata za jimbo hilo, zikiwemo Chamazi, Mianzini, Kilungule, Charambe, Mbagala, Kuburugwa, Kijichi na Mbagala Kuu litaisha.

Akijibu swali hilo, Judith alisema changamoto ya kukatika umeme mara kwa mara katika jimbo hilo unatokana na kuzidiwa kwa Kituo cha Kupoza Umeme cha Mbagala.

“Serikali inatarajia kufunga nyaya zenye uwezo mkubwa katika njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 132 kutoka Kinyerezi hadi Mbagala kupitia Gongo la Mboto.

“TANESCO inaendelea na usimamizi wa mradi wa kuipatia Wilaya ya Mkuranga kituo kikubwa cha kupozea umeme chenye uwezo wa MVA 240 eneo la Dundani na kuacha utegemezi katika Kituo cha Mbagala.” alisema.

 

error: Content is protected !!