Diamond achambua miaka 60 ya Uhuru na Mawaziri

HomeBurudani

Diamond achambua miaka 60 ya Uhuru na Mawaziri

Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameshiriki katika mjadala wa miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania, Tulipotoka, tulipo na tunapoelekea na kuweza kuchambua mafanikio ya kiuchumi, kisiasa , kidiplomasia na utamaduni pamoja na wadau mbalimbali.

Diamond alisema kwamba katika miaka 60 ya Uhuru akiwa kama msanii ameshuhudia mafanikio mbalimbali, yakiwemo ya Watanzania kuzidi kuwa kileleni katika tuzo zinazotolewa Afrika kwa kushika nafasi za juu, jambo ambalo limetokana na mifumo thabiti iliyowekwa na serikali katika kuongeza thamani sekta ya sanaa.

Pia, alitoa pongezi kwa Rais Samia kwa kuboresha mazingira mazuri ya diplomasia kwani yanaendelea kugungua sekta ya sanaa kwa kufanya kazi na mataifa mbalimbali duniani.

Baadhi ya watu walioshiriki mjadala huo ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge , Ajira , Vijana na Watu Wenye Ulemavu, alisema katika miaka 60 ya Uhuru kuna ongezeko la vijana wasomi, ambao wametokana na usimamizi mzuri wa serikali katika sera ya mapambano ya adui ujinga, maradhi na umasikini, ambayo ilikuwa falsafa ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

error: Content is protected !!