Karani akutwa amelewa Musoma

HomeKitaifa

Karani akutwa amelewa Musoma

Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujaribu kukwamisha Sensa ya Watu na Makazi mjini Musoma.

Mratibu wa Sensa wa Manispaa ya Musoma, Joseph Ochora amemtaja karani wa sensa, Thomas Ndyetabura kwamba anashikiliwa na polisi tangu juzi kwa kuhesabu kaya moja tu kutwa nzima, baadaye kukutwa akiwa amelewa.

Kwa mujibu wa Ochora karani huyo alitakiwa kuhesabu kaya kati ya 20 hadi 30 kwenye Kata ya Kwangwa, lakini baada ya matendo hayo nafasi yake ikatolewa kwa karani mwingine na kazi inaendelea.

“Changamoto nyingine imetokea Kata ya Kitaji, Barabara ya Shaban Nyumba Namba 28, ambapo kaya moja ilikataa kuhesabiwa, tumewakabidhi polisi,” amesema Ochora.

error: Content is protected !!