Yanga SC yashangazwa kutoalikwa mkutano wa CAF

HomeKitaifa

Yanga SC yashangazwa kutoalikwa mkutano wa CAF

Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema umeshangazwa kwanini hawakupewa mwaliko wa kuudhuria mkutano wa 44 wa Shirikisho la CAF.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Yanga wakili Simon Patrick amesema walilazimika kufuatilia mkutano huo kupitia mitandao ya kijamii baada ya kukosa mwaliko.

Simon ameongeza kuwa, ingawa mkutano huo ni wa CAF lakini ilipaswa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutambua nafasi ya Yanga kushiriki kwenye mkutano huo na kupewa mwaliko.

“Bahati mbaya hatujajua kipi kimetokea na sisi (Yanga) kukosa mualiko, tuliamua kutumia fursa ya teknolojia tuweze kufuatilia mkutano huo.” amesema.

Simon amekiri kuwa klabu ya Yanga ambao ni mabingwa wa nchi walitamani kuwepo katika mkutano huo uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soko Duniani (FIFA), Giovanni Vincenzo.

 

error: Content is protected !!