Watu wanne wamefariki Kenya, vurugu za Uchaguzi Mkuu

HomeKitaifa

Watu wanne wamefariki Kenya, vurugu za Uchaguzi Mkuu

Licha  ya  juhudi za wagombea wa viti mbalimbali nchini Kenya kulaani vurugu na kuwataka wafuasi wao kuwa watulivu wakati shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea, kumeripotiwa baadhi ya vurugu zilizosababisha vifo vya watu wanne.

Uchaguzi Mkuu wa Kenya ulifanyika Agosti 9, 2022, kura za urais zinaendelea kuhesabiwa huku mchuano mkali ukiwa kati ya Raila Odinga na William Ruto.

​Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti vurugu katika baadhi ya maeneo ikiwemo Kimilili ambapo mshindi wa kiti cha ubunge wa kaunti ya Kimilili Dismas Barasa anashtakiwa kwa kosa la mauaji ya Brian Olunga, mlinzi wa mpinzani wake Brian Khaemba.

Kwa mujibu wa blogu ya Tuko imesema Agosti 10, 2022 Dismus alitoa bastola iliyomlenga na kumpiga risasi ya paji la uso msaidizi huyo aliyefariki wakati akipatiwa matibabu.

Mbunge huyo alikasirishwa na kitendo cha mgombea mwenzake kujaribu kuondoka katika kituo cha kupiga kura.

Pia Kamanda wa Polisi Kaunti ya Migori, Mark Wanjala amethibitisha mtu mmoja (25) alifariki jana jioni baada ya kupigwa na kitu kizito kichwani wakati wa ghasia za uchaguzi zilizozuka katika kaunti ndogo ya Uriri.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Standard Media, August 10, 2022 huko Nyanza kijana mmoja aliyetambulika kama Michael Odhiambo (30), aliuawa katika jimbo la uchaguzi la Rangwe, Kaunti ya Homa Bay baada ya ghasia kuzuka.

Waliosababisha mauaji hayo walivamia boma la wazazi wake katika kijiji cha Ang’iro, kata ya Kochia na kumwacha na majeraha mabaya. Alifariki muda mfupi baadaye.

Kwingineko, mtu mmoja ambaye hakujulikana  mara moja alipigwa risasi ila akufariki dunia katika eneo bunge la Bonchari, Kaunti ya Kisii, wakati makundi hasimu yakipambana Jumatatu usiku.

Licha ya visa hivyo vichache vya vurugu, uchaguzi huo umefanyika kwa amani  katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.

error: Content is protected !!