Wauzaji wa nyeti za binadamu wakamatwa

HomeKitaifa

Wauzaji wa nyeti za binadamu wakamatwa

Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, ACP Richard Abwao amesema wanawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji wa viungo vya binadamu ikiwemo nyeti za binadamu.

Miongoni mwa watuhumiwa hao wawili ni waganga wa jadi ambao ndio wanunuzi wa viungo hivyo, na  wengine wawili huenda kutafuta viungo hivyo kwa kuua watu na kisha kuviuza kwa waganga wa kienyeji.

ACP Abwao anasema baada ya kufanya nao mahojiano vijana hao walisema hufanya mauaji kwa kutumia kitu chenye ncha kali ili waweze kukinga damu kwenye chupa.

Damu hiyo wanaiuza kwa waganga wa kienyeji kwa Tsh 600,000 pia wanauza viungo ambavyo bei yake huwa ni makubaliano kati yao na waganga wa jadi.

Msako wa kuwatafuta wauaji mkoani Tabora ulianza January 21 kutokana na  kifo cha mwanafunzi wa shule ya Msingi Tutuo, mwenye wa miaka 14.

Msako huo ulifanyika ili kuwapata wauaji na hatimaye wakafanikiwa kuwakamata watu wanne lakini bado msako unaendelea ili kubaini watu wengine ambao wanashirikiana nao.

“Baada ya tukio la mauaji ya mwanafunzi wa shule ya Msingi Tutuo , tulianza operesheni hii na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne hadi tutakapofanikiwa kuuzima mtandao wa wahalifu” alisema ACP Richard Abwao.

error: Content is protected !!