Jamii ya wamasai yashukuru kujengewa madarasa

HomeKitaifa

Jamii ya wamasai yashukuru kujengewa madarasa

Wakazi wa kitongoji cha Umasaini kilichopo nje kabisa ya mji wa Pangani, wameishukuru Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia madarasa katika shule shikizi ya iliyopo katika kitongoji chao.

Kitongoji cha Umasaini kipo katika eneo lililojitenga na mji wa Pangani, ambapo watoto walilazimika kusoma katika vibanda vikuukuu ambavyo hutumika pia kama sehemu za ibada.

“Ilikuwa tunapata shida, watoto wetu wanapokwenda kusoma, wanaenda kusomea mbali. Wanasomea Ushongo, Ushongo pale kuna maddimbwi ya maji, kuna mifereji ya maji. Sasa watoto wetu tukawa tunapeleka tu kwa shida kwa sababu na sisi tunataka elimu. Rais Samia tunashukuru ni Mama mwenzetu, ameingi kwenye kiti sisi tukapata huduma kubwa sana.” amesema Katarina Baraka ambaye ni mkazi wa kitongoji cha Umasaini.

Wilaya ya Pangani imepokea shilingi milioni 560 katika mgao wa fedha za Mpango wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19, kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 28. Shule shikizi ya Umasaini ni kati ya maeneo yaliyonufaika na madarasa hayo.

error: Content is protected !!