Dkt Samia: Nataka matokeo kwa wananchi sio michakato inaendelea

HomeKitaifa

Dkt Samia: Nataka matokeo kwa wananchi sio michakato inaendelea

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewaapisha mawaziri na naibu mawaziri wake, huku akiwaeleza katika muhula wa pili wa Serikali yake, anataka kuona matokeo kwa wananchi sio ofisini.

Amewaambia mawaziri hao kuwa, katika utendaji wao hatapenda kusikia neno kuwa ‘tunaendelea’ au ‘mchakato upo mbioni’ bali matokeo pekee kwa wananchi.

Mkuu huyo wa nchi, ametoa kauli hiyo leo, Jumanne Novemba 18, 2025 alipozungumza wakati wa hotuba yake ya kuwaapisha mawaziri na naibu mawaziri Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

“Tukikubaliana mradi ni matokeo kwa wananchi si ofisini kwako, tumefikia hapa, bado hapa hapana…matokeo kwa wananchi kwa muda tutakaokubaliana,” amesema Dkt Samia.

error: Content is protected !!