Kutokana na ongezeko la bei ya mafuta ghafi tangu mwezi mei 2020 ambapo bei imeongezeka mara mbili kutoka wastani wa dola za kimarekani 32 kwa pipa mwezi Mei 2020 na kufikia dola za kimarekani 86 kwa pia mwishoni mwa mwenzi oktoba 2021.
Ili kuepusha madhara ya ongezo la bei za mafuta katika uchumi na maisha ya wananchi, mwezi Julai 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliagiza hatu mbalimbali zichukuliwe kwa lengo la kupunguza bei za mafuta ili wananchi wapate nafuu.
Kupitia Wizara ya Nishati inayoongozwa na Waziri January Makamba, aliwasilisha mapendekezo ya kupunguza tozo na ada zinazotozwa na taasisi za Serikali katika bidhaa za mafuta. Kufuatia jitihada hizo za nyinginezo, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za mafuta ya petroli kwa mwezi Novemba 2021.
Cap Prices for Petroleum Products wef 3rd November 2021-Kiswahili