Mtandao wa Facebook umechukua uamuzi wa kubadili jina lake lililozoeleka na wengi na kujiita ‘Meta’. Facebook imesema kuwa kufanya hivyo ni moja ya harakati zake katika kutanua wigo wa huduma zake kuwa zaidi ya mtandao wa kijamii, bali hata huduma za ‘Virtual Reality’.
Facebook imeweka wazi kuwa, mabadiliko hayo hayataathiri majina ya mitandao yake kama Facebook, Instagram na WhatsApp, bali itabadili jina la kampuni mama pekee, kutoka Facebook kuenda Meta.
Mabadiliko yamekuja siku chache baada mfulilizo wa sifa mbaya ambazo zimeathiri kwa kiasi kikubwa kampuni hiyo na skendo za juu ya matumizi mabaya ya taarifa za watu. Mathalan, kuvujishwa kwa nyaraka za siri na moja ya aliyekuwa mwajiriwa katika kampuni hiyo.
Mwajiriwa huyo kwa jina Frances Haugen aliishutumu Facebook kuwa inajali faida zaidi kuliko taarifa za watu. Mwaka 2015 Google walichukua uamuzi kama huo kuweka kampuni zake zote chini ya jina la Alphabet, ambapo hata hivyo jina hilo bado halijakaa vichwani mwa watu.