Tanzania na Malawi ni mataifa yenye historia kongwe katika nchi za maziwa makuu. Mataifa haya mawili bega kwa bega yalishirikiana katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Ushirikiano huu umekuwa chachu kubwa katika kuchochea maendeleo ya mataifa yote mawili.
Biashara kati ya Tanzania na Zambia imeimarika zaidi tangu 2019 baada ya nchi hizi mbali kufungua matumizi ya mpaka wa Tunduma na Nakonde uliogharimu kiasi cha dola za kimarekani million 6.5. Mpaka huo umeongeza thamani katika biashara baina ya nchi hizi. Takwimu zinaonesha kuwa biashara kati ya Zambia na Tanzania imeongezeka kutoka dola milioni 89 mwaka 2010 hadi dola milioni 265 mwaka 2019.
Mpaka wa Tunduma na Nakonde umeimarisha zaidi sekta ya usafirishaji. Kabla ya kujengwa kwa mpaka kati Tunduma na Nakonde ilichukua siku tatu hadi nne kuingia Zambia kutokea Tanzania, lakini baada ya ujenzi wa mpaka hivi sasa inachukua siku moja tu.
Tanzania na Zambia zinahistoria komavu kwenye masuala ya biashara. Moja ya mradi mkubwa wa kihistoria ambao ni ishara ya udugu kati ya Tanzania na Zambia ni ujenzi wa reli ya TAZARA (Tanzania Zambia Railway Authority) mnamo mwaka 1970 kwa ushirikiano kutoka serikali ya China. Reli za TAZARA inaanzia mashariki mwa Tanzania kuunganisha bandari ya Dar es Salaam na mji wa Kapiri Mposhi kule Zambia. Reli ya TAZARA imeingiza mapato kiasi cha dola za kimarekani milioni 44.10 mwaka 2016/2017.
COMMENTS