Flaviana Matata atema nyongo

HomeMatangazo

Flaviana Matata atema nyongo

Flaviana Matata, mwanamitindo maarufu wa Tanzania na duniani ambaye mwaka 2013 jarida la Forbes la Afrika liliandika kwamba ni miongoni mwa wanamitindo saba ambao wanaingiza kipato kikubwa barani Afrika. Flaviana amesema jamii iache kuwadhihaki wanawake mara baada ya kuvunjika kwa ndoa zao na kupewa talaka kwani ni mengi wanapitia mpaka kufikia maamuzi kama hayo.

Flaviana ameongea hayo baada ya kuangalia mahojiano ya msanii kutoka nchi Uingereza, Adele wakati anahojiwa na Oprah Winfrey ambapo msanii huyo alielezea hali aliyopitia baada ya kuachana na mume ambaye alidumu naye kwa miaka 8.

Mwanamitindo huyu ameandika kwenye ukurasa wake Instagram jinsi alivyodhihakiwa na watu wengi mwaka 2019 alipoachana na mume wake, huku akisema jamii ilikua ikimsema kwenye mitandao kama ameuwa mtu au kufanya jambo baya bila wao kujua sababu zinazopelekea talaka hiyo.

Pia Matata amewasihi watu kutowadhihaki na kuwasema na kuwalaumu wanawake pale ndoa zinapovunjika na kuwatupia lawama kwamba wao ndio chanzo huku akimalizia kusema kwamba sio kila mtu anapenda kufunga ndoa na kuachana lakini kuna sababu ambazo haziwezi kuelezeka kwenye jamii.

error: Content is protected !!