Hii hairuhusiwi

HomeKitaifa

Hii hairuhusiwi

Taarifa kwa Umma kutoka Wizara ya Maliasili

JAMBO HILI HALIRUHUSIWI NDANI YA HIFADHI ZETU!

Jambo hili tunaweza kulifurahia lakini ni hatari na HALIKUBARIKI. Chita ni mnyamapori mwenye tabia kupanda juu ya magari hususani yale yanayokua yamefungua paa yakiwa yamebeba watalii ndani ya hifadhi. Jambo hili ni hatari kwa usalama na HALIRUHUSIWI kutokana na uwezekano mkubwa wa mnyamapori huyo kudondokea ndani ya gari na kusababisha madhara makubwa ikiwemo kujeruhi wageni au yeye mwenyewe kujeruhiwa pindi anapojaribu kupanda juu ya paa.

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUEPUKA CHITA KUPANDA JUU YA MAGARI YA WATALII.

Pale dereva unapobaini Chita analikaribia/wanalikaribia gari lako au kulisogelea, washa gari lako na kuliondoa taratibu na kwa uangalifu mkubwa pia chukua tahadhari kwa hakikisha usalama wa wageni walio ndani ya gari.

Wakati mwingine gari la wageni lililosimama linaweza kuzungukwa na idadi kubwa ya Chita, hali hiyo inapotokea dereva/muongoza wageni anapaswa kuhakikisha usalama wa wageni wake pamoja na kuangalia mazingira ya nje kabla ya kuondoa gari ili kuepusha madhara ya kuwagonga na kuwajeruhi Chita waliolifikia gari.

error: Content is protected !!