Hii ndio mitaa 4 iliyotengwa kwa machinga wa Kariakoo

HomeKitaifa

Hii ndio mitaa 4 iliyotengwa kwa machinga wa Kariakoo

Uongozi wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga, umetenga mitaa minne katika eneo hilo ambayo itatumika maalum kwa ajili ya shughuli za wajasiriamali hao hii ni kutokana na uhaba wa maeneo ya kufanyia biashara ndogo katika eneo la Kariakoo.

Makamu Mwenyekiti wa wafanyabiashara Taifa, Stephen Lusinde alisema mitaa iliyotengwa ni Kongo, Nyamwezi, Swahili na Sikukuu huku akibainisha kuwa maeneo hayo yatatumika kipindi cha neema cha siku 12 zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla.

> Vurugu za Machinga Kariakoo, Mkuu wa Mkoa DSM atoa neno

“Changamoto za hapa na pale zipo kwa sababu sisi ni binadamu, lakini ukizingatia mtu ana miezi sita au mwaka katika eneo, kumhamisha kidogo ni changamoto lakini tunaendelea kutoa elimu ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanikiwa.” Alisema Lusinde

Aidha alitoa ufafanuzi ugomvi uliojitokeza juzi katika eneo la Kariakoo wakati wakitimiza majukumu yao, akibainisha kuwa vurugu zilifanywa na vijana wahuni na sio wafanyabiashara.

“Kulikuwa kuna watu waliotaka kutumika, sisi hatuwezi kutafsiri sana kuwa ni kisiasa au ni kwa namna gani kuhakikisha wanaharibu hili zoezi ambalo lina dhamira njema, walikuwa wanawarushia mawe viongozi wa machinga ili kutaka kuanzisha tafrani, hivyo ieleweke kuwa watu hao sio wamachinga halisi” Alisisitiza Lusinde

error: Content is protected !!