Ijue Siri ya wanawake wa Kusini mwa Afrika kuwa maumbo namba 8

HomeElimu

Ijue Siri ya wanawake wa Kusini mwa Afrika kuwa maumbo namba 8

Wanawake wa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika maumbile yao ni tofauti na wanawake wa nchi nyingine. Wanawake kutoka nchi kama Botswana, Namibia, Swaziland pamoja na Lesotho maumbo yao kwa lugha ya vijana huitwa namba 8. Ipo siri kubwa nyuma ya maumbile haya ambayo yamekuwa kivutio kikubwa kwa wanaume wengi barani Afrika na duniani.

Siri yake ni nini hasa?

Maumbile haya si yakutengeneza, bali ni asilia ambayo husababishwa hasa mlundikano wa mafuta (fat) katika maeneo ya makalio na mapaja. Kwa lugha ya kisayansi kitendo huitwa ‘Steatopygia’, neno hili ni muunganiko wa maneno mawili ya kigiriki (steato+pugḗ) ‘steato’ ikiwa na maana ya mafuta na ‘pugḗ’ ikiwa ni eneo la nyuma au chini mnyama au ndege.

Kwa kuwa maumbile haya hubebwa kwenye vinasaba vya watu, hivyo huweza kurithishwa kutoka kwa mzazi kuenda kwa watoto. Jamii ya watu wa kabila la Khoisan Kusini mwa Afrika ndio watu maarufu kwa kuwa maumbile haya ya kuvutia. Jamii nyingine ni ‘Pygmies’ wa Afrika ya kati pamoja na ‘Andamanese’ kutoka Ghuba ya Bengal, Kusini mwa Bara Asia. Mara nyingi maumbile haya hurithishwa kwa Wanawake, na aghalabu kwa Wanaume.

Kwa wasichana wa kabila la Khoisan, maumbile haya huanza kuonekana wakiwa bado watoto kabisa, na huchomoza moja kwa moja baada ya kushika ujauzito wa kwanza. Kwa kabila la Khoisan hii ni ishara ya urembo.

Maeneo ambako Wanawake hawa wenye maumbo namba 8 yanakuwa na joto kali, na huwasaidia kuvumilia njaa kwa kuwa miili yao huweza kutumia mafuta yaliyomo kuendelea kustahamili muda mrefu.

error: Content is protected !!