Jinsi ya kujikinga na homa ya Mgunda

HomeKitaifa

Jinsi ya kujikinga na homa ya Mgunda

Licha ya ugonjwa huo kutokuwa tishio bado Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameitaka jamii kuchukua tahadhari za kujikinga ikiwemo kuepuka kunywa na kugusa maji  yaliyochafuliwa na wanyama wenye maambukizi,cudongo au chakula cha wanyama wenye maambukizi.

Tahadhari nyingine ni  kunywa maji safi na salama yaliyochemshwa na kutibiwa, pamoja na kuchukua hatua za mapema za kufika kwenye kituo cha afya endapo utajihisi una dalili za ugonjwa huo ambazo ni pamoja  mwili kuchoka, homa, kuvuja damu na kichwa kuuma.

“Dalili nyingine ni macho kuvilia damu, kuumwa misuli, mwili kuwa wanjano kutoka damu puani kukohoa damu na kusikia kichefuchefu,” alisema  Waziri Ummy.

Aidha wizara imewataka wananchi kutoa taarifa za wagonjwa wanaoonyesha dalili za ugonjwa huo katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Pia amewasisitiza waganga wakuu wa mikoa na wilaya  kufufua timu za ufuatiliaji wa magonjwa na tetesi za magonjwa majumbani na kuhakikisha mgonjwa anapelekwa kituo cha afya, kupimwa na kugundua ugonjwa kwa haraka.

error: Content is protected !!