Vibanda ndani ya soko la Karume mkoani Dar es Salaam vimeungua kwa mara nyingine, alfajiri ya saa 11 leo, Aprili 8, 2022.
Kamanda Elisa Mugisha wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Ilala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema vikosi vya uokoaji vimeudhibiti moto huo ulioathiri baadhi ya vibanda katika soko la Karume.
Januari 16 mwaka huu moto mkubwa ulizuka na kuteketeza soko la Karume na leo ikiwa ni mara ya pili ndani ya mwaka mmoja.
Mbali na kuungua kwa vibanda hivyo hakuna mali zilizoteketea wala vifo.