Mataifa mengi ya Afrika kutokana na changamoto za kiuchumi na teknolojia ndogo, bado hayajaweza kuvuna rasilimali muhimu sana inayoweza kupatikana kwenye kinyesi cha binadamu. Hii itakushangaza, lakini ndio ukweli. Hizi ni faida 5 muhimu za kinyesi cha binadamu.
1. Huzalisha Nishati
Gesi aina ya ‘Methane’ ni gesi ambayo hupatikana kwenye kinyesi cha binadamu. Gesi hii ni muhimu sana kwa kupikia hata kuendeshea vyombo vya moto kama magari. Mnamo 2015 kampuni ya FirstGroup ya Uingereza ilizindua gari ya kwanza inayotumia nishati kutoka kwenye kinyesi cha binadamu.
2. Mafuta ya “Rocket”
Wanaanga wanaofanya safari za kwenye mwezi hivi sasa hawahitaji tena kutumia mifuko maalumu kuhifadhi vinyesi vyao. Hii ni baada ya Chuo Kikuu cha Florida kugundua njia ambayo kinyesi kinaweza kutumika kuzalisha mafuta ambayo yanaweza kutumika kama nishati ya kuendeshea ‘rocket’. Ilikadiriwa kwamba, lita 290 za methane zinaweza kuzalishwa kutoka kwa Mwanaanga mmoja na kiasi hicho kutosha kabisa kutumika kurudisha ‘rocket’ duniani.
3. Kinga dhidi ya miale
Katika moja ya dira ya mataifa makubwa katika sayansi ya anga ni kufanya mwanadamu aweze kuishi kwenye sayari zaidi ya moja. Hivyo sayari ambayo inatazamiwa binadamu kuishi ni sayari ya “Mars”. Lakini huko kuna miale hatari ambayo inaweza kusababisha saratani kwa haraka. Kwa sasa, suluhisho la kisayansi lililopo ni kutumia kinyesi cha binadamu kutengeneza teknolojia ambayo itaweza kupunguza ukali wa miale hii.
4. Mbolea
Takribani jamii na tamaduni zote duniani wametumia kinyesi kwa kazi hii ya uzalishaji wa chakula. Zipo kampuni nyingi Ulaya kama vile Tiger Toilet ambayo kazi yake ni kukusanya kinyesi cha binadamu, kukitibu kisha kutengeneza mbolea ambayo ni rahisi na salama kwa matumizi ya binadamu.
5. Mgodi wa dhahabu
Wanasayansi wanatafuta utaratibu wa kuvuna madini kama dhahabu, fedha, platinum, shaba pamoja na titaniam ambayo yanaweza kupatikana kwenye kinyesi cha binadamu. Chuo Kikuu cha Arizona nchini Marekani kilitoa utatifi unaosema kwamba, kinyesi cha Wamerekani wote kwa Mwaka, kinaweza kutoka madini yenye thamani ya dola milioni 13 za kimarekani.