Kiongozi mkuu wa Hamas auawa

HomeKitaifa

Kiongozi mkuu wa Hamas auawa

Kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas la Palestina Ismail Haniyeh ameuwa katika mji mkuu wa Iran, Tehran, vyombo vya Habari vya serikali ya Iran vimesema.

Hamas imesema Haniyeh ameuawa katika shambulio la Israel kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian.

Imesema mauaji hayo hayatapita bila kujibiwa.

Mauaji hayo yametokea wakati hali ya wasiwasi ikizidi Mashariki ya Kati, huku mapigano kati ya Israel na kundi la Hezbollah la Lebanon yanayozidi yakitishia kuenea kwa vita eneo hilo na Hamas ikipambana na jeshi la Israel katika ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israeli limesema halijibu ripoti za vyombo vya Habari vya nje ingawa maafisa waandamizi awali waliapa kuiangamiza Hamas na uongozi wake kujibu shambulio la kundi hilo Oktoba 7, 2023 nchini Israel.

Julai 30, Israel imesema shambulio lake jijini Beirut limemuua kamanda mwandamizi wa Hezbollah, aliyepanga shambulio la roketi katika vilima vya Golan vinavyokaliwa na Israel lililoua Watoto 12.

Aprili mwaka huu mashambulio ya Israel katika ukanda wa Gaza yaliua watoto watatu wa Haniyeh na wajukuu wake wanne.

error: Content is protected !!