Kiwanda cha kuunganisha pikipiki na bajaji kujengwa Chamwino

HomeKitaifa

Kiwanda cha kuunganisha pikipiki na bajaji kujengwa Chamwino

Kiwanda kipya cha kwanza cha kuunganisha pikipiki na bajaji kitajengwa katika Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.

Kiwanda hicho kitajengwa mkoani homo kama sehemu ya pili ya utekelezji wa mpango wa ushirikiano baina ya mkoa huo na wawezekezaji wa Kampuni ya Lifan Group na Tamoba kutoka nchini China.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Katika Tawala Msaidizi Seksheni za Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mwajabu Nyamkomora alisema Wilaya ya Chamwino imejiandaa kupokea mradi huo kwani tayari wilaya hiyo imeandaa eneo la ekari 100 kwa ajili ya uwekezaji.

“Katika kuhakikisha uwekezaji huo unafanikiwa, serikali imeshaandaa mazingira wezeshi mkoani humo na hasa katika wilaya hiyo kwa ajili ya kutoa nafasi kwa sekta binafsi kuwekeza,” alisema Mwajabu.

Wawekezaji hao kutoka China wamefika nchini hadi mkoani Dodoma na kufanya mazungumzo kuhusu nia yao ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda hicho muhimu nchini.

Aidha, wawekezaji hao pia walihamasishwa kutumia fursa nyingine nyingi kuwekeza katika mkoa huo.

error: Content is protected !!