Diamond Platnumz, msanii machachari kutoka Tanzania, muazilishi, mmiliki na mkurugenzi wa kampuni inayojishughulisha na maudhui ya muziki ya WCB. Diamond Platnumz ni ‘Philanthropist’, yaani yeye ni mtu anayejitoa sana kwa ajili ya jamii kwa kutoa misaada kwa makundi mbalimbali katika jamii.
Tarehe 7 Desemba 2021 tovuti maarufu ya Gluesea ilitoa taarifa katika mtandao wake kuonesha utajiri aliokuwa na Diamond Platnumz mwaka 2021. Tovuti hiyo inaeleza kuwa Diamond Platnumz ana utajiri wa dola za Kimarekani milioni 10, sawa na shilingi bilioni 21.5 za Kitanzania.
Diamond ni msanii mashabiki wengi zaidi Afrika Mashariki na kati, na pia ndiye msanii anayekusanya mapato mengi zaidi katika kuuza kazi zake katika mitandao.
Tovuti moja ya Afrika Kusini inaeleza kuwa, Diamond Platnumz anaingia shilingi milioni 7 kwa siku kwenye kazi zake za muziki pekee, hivyo kufanya kuingiza shilingi milioni 730 kwa mwaka. Mwaka 2018, Mtandao wa Ghafla wa Kenya ulieleza kuwa Diamond aliingiza Shilingi bilioni 1 kwenye shows zake za Afrika, Ulaya pamoja na Marekani.
Diamond Platnumz miaka ya nyuma na 2021 amefanya kazi kama balozi na kampuni kama
1. Mziiki
2. Itel
3. Pepsi
4. Belaire
5. Coral Paint
6. Parimatch
7. Red Gold
8. Nice One
9. GSM
10. Vodacom
Fununu zinasema kwamba deal ya Diamond ya mtandao wa Mziiki (online music streaming) ina thamani ya dola milioni 5, sawa na bilioni 10 za kitanzania.
Deal ya itel, kampuni ya simu inayofanya vizuri barani Afrika inasemekana kwamba amelipwa kati ya dola 50,000 – 150,000 (TZS milioni 120 – 320).
Deal yake na Pepsi unaambiwa ni kubwa sana, Pespsi wameweka hela nyingi sana na vyanzo vyetu vya ndani vimeshindwa kupata taarifa hiyo, ingawa kwa ujumla ni hela nyingi zaidi ya dola 500,000 za kimarekani.
Habari za ndani zinadai kwamba kwenye deal ya Belaire Diamond Platnumz amelipwa dola 500,000 za kimarekani, na Kampuni ya Rangi la Coral Paints imemlipa 600 milioni za kitanzania na kampuni ya Betting ya Parimatch imemlipa dola 70,000 za kimarekani.
Bado Diamond ananyumba nyingi sana hapa Tanzania na nje ya nchi ambazo zinamuingizia mkwanja mrefu sana. Maisha ya Diamond Platnumz kila kinachomzunguka na anayemzunguka ni mapato. Kupitia jina lake watu wengi wananufaika na hata kupitia watu hao, yeye ananufaika zaidi. Itoshe kusema kwamba kwa sasa Diamond Platnumz ni msanii mwenye mkwanja mrefu zaidi Afrika Mashariki na kati.