Leseni maalum za uzalishaji chumvi mbioni kuanza

HomeKitaifa

Leseni maalum za uzalishaji chumvi mbioni kuanza

Serikali ipo mbioni kutambulisha leseni mpya ya uzalishaji wa chumvi kwa lengo la kuiondoa bidhaa hito katika kundi la madini mengineyo.

Hayo yalisemwa jijini Dodoma jana katika Kikao cha Waziiri wa Madini, Anthony Mavunde na uongozi wa Chama cha Wazalisha Chumvi Tanzania (TASPA) chenye lengo la kuboresha sekta ya madini kupitia tasnia ya chumvi.

“Rais Samia Suluhu Hassan ametupa maelekezo mahsusi kuwezesha wachimbaji madini na wazalishaji madini chumvi nchini wanachochea ukuaji wa sekta ya madini.

“Serikali imesikia kilio chenu cha muda mrefu cha uwepo wa leseni moja ya uzalishaji wa chumvi ambayo itasaidia kumuendeleza mzalishaji chumvi kwa kupunguza gharama za uzalishaji na kuyaondoa madini chumvi katika kundi la madini mengineyo,” alibainisha.

Naye, Mwenyekiti wa TASPA, Hawa Ghasia, aliipongeza Wizara ya Madini kwa utaratibu wa kuwasikiliza wadau kisha kutafuta suluhisho ya changamoto zao.

error: Content is protected !!