Machinga Dar es Salaam wakumbushwa bado siku 1 tu

HomeKitaifa

Machinga Dar es Salaam wakumbushwa bado siku 1 tu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema kuwa ifikapo siku ya kesho ndio mwisho kwa wanaofanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa kutokana na muda wa siku 12 alizoongeza kufikia kikomo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam RC Makalla ameeleza kuwa zoezi la kuwapanga vizuri Machinga katika mkoa huo linakwenda vizuri na amewataka wafanyabiashara wanaofanya biashara maeneo yaliyokatazwa hususani Kariakoo kufika Soko la Machinga Complex kwa ajili ya kupatiwa nafasi kutokana na Soko hilo kusaliwa na nafasi 2,400 zinazopaswa kutumiwa na wafanyabiashara wadogo.

> Hii ndio mitaa 4 iliyotengwa kwa machinga Kariakoo

RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko hilo na kueleza kuwa mpaka sasa zaidi ya wafanyabiashara 2,200 wamepatiwa maeneo ya kufanyia biashara na wanafurahia biashara zinakwenda vizuri sokoni apo.

Aidha RC Makalla amesema Serikali imedhamiria kutatua changamoto zote za kibiashara kwenye maeneo waliyopelekwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuelekeza LATRA kufikisha huduma ya usafiri wa ‘Daladala’ kwenye maeneo hayo ikiwemo Soko la Machinga ili kuchochea biashara.

error: Content is protected !!