Madini ya Afrika yanayotumika kutengeneza simu

HomeKitaifa

Madini ya Afrika yanayotumika kutengeneza simu

Utajiri mkubwa wa Afrika upo kwenye ardhi yake, ardhi yenye rutuba kustawisha mimea, lakini ardhi hiyohiyo yenye kuficha vito vya thamani na vya upekee kwa bara hili.

Afrika ina nafasi kubwa katika ulimwengu wa utandawazi na teknolojia hasa katika vifaa vya umeme ikiwemo simu za mkononi ambazo mbali na kutengenezwa nje ya Afrika nyingi hutegemea kifaa kimoja kutoka Afrika ili simu iweze kufanya kazi.

Coltan ni madini ambayo ulimwenguni kote yanapatikana Congo kwa 80%. Madini haya hutengeneza vifaa vyenye kupunguza moto kwenye vifaa vya kielektroniki. Congo ndio nchi inayoongoza kwa usambazaji wa Coltan ndani na nje ya Afrika.

Ingawa Coltan haiongelewi sana, Coltan huzalisha ‘tantalum ambayo ndio kiungo muhimu katika vifaavya umeme na bila hiyo pengine usingeweza kuitumia simu yako. Si tu kwenye simu bali kwenye laptop na hata kwenye kuzalisha umeme unaoendesha upanga wa ndege.

error: Content is protected !!