Mbinu 5 za kuzuia simu yako isidukuliwe

HomeElimu

Mbinu 5 za kuzuia simu yako isidukuliwe

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi kwa watumiaji wa Kompyuta mpakato na simu kutoka nchi mbalimbali kuhusu wadukuzi kudukua taarifa zao. Ripoti zinaonesha wadukuzi hao wanalenga taarifa muhimu kama za benki, mitandao ya kijamii na hata taarifa za siri za kikazi.

Wadukuzi wapo wa aina tofauti kuna wale wanaotaka kukudhalilisha, kuna wanaotaka kuiba pesa zako na wale wanaotaka kujua mwenendo wa kampuni fulani hivyo basi ili kuepuka kudukuliwa taarifa zako zingatia mambo yafuatayo

1. Pakua taarifa kwenye vyanzo vya kuaminika
Watu wengi wanapenda kupakua taarifa mbalimbali kutoka katika programu tumishi zisizo salama. Watumiaji wa simu zenye mfumo wa “android” wana programu nyingi za kupakua taarifa hivyo ni vyema ukawa makini pindi ufanyapo hivi kwani unaweza kukuta unadukuliwa bila kujua.

2. Usipende kuunganisha ‘wi-fi’ za bure
Watanzania wengi tunapenda kutumia intaneti za bure na kujiunga bila kuangalia kama ni salama au si salama, kwa kufanya hivi unaweza kukuta umedukuliwa bila wewe kujua

3. Weka neno la siri kwenye vifaa vyako
Kama wewe ni mtumiaji wa simu na kompyuta mpakato ni vyema ukawa unaweka neno la siri ili kulinda kifaa chako kisiduliwe kwani bila kufanya hivyo inakuwa rahisi kwa wadukuzi kupata taarifa zako.

               > Tumia mbinu hizi ili bando la intaneti lisiishe haraka kwenye simu yako

4. Sasisha (Upgrade) kompyuta na simu mara kwa mara
Hakikisha una-upgrade kompyuta mpakato yako na simu mara kwa mara ili ziwe salama na ndio maana makampuni hutoa matoleo mapya ya kusasisha vifaa hiyo ili kuviweka salama.

5. Hakikisha unazima kamera na sensa za simu na kompyuta
Ndio maana simu yako inaitwa simu janja kwani ina uwezo wa kufanya mambo mengi, unashauriwa kuzima sensa na kamera ili isiwe rahisi kwa wadukuzi kujua na kuona nini unafanya.

Pamoja na ushauri huu wataalamu wa teknolojia wanaeleza kuwa endapo mdukuzi ataamua kutumia muda wa kutosha pamoja na uwekezaji (resource) za kutosha kutaka kukudukua basi kuna uwezekano mkubwa akafanikiwa. Ndio maana kuna wakati wadukuzi walidukua ukurasa wa Facebook wa mmiliki wa Facebook Mark Zuckerberg. Hivyo utumiapo mitandao na intaneti kwa ujumla chukua tahadhari lakini tegemea lolote wakati wowote

error: Content is protected !!