MBUNGE Jimbo la Mbarali mkoani Mbeya, Francis Mtega amefariki dunia.
Taarifa iliyotolewa na Bunge leo Julai Mosi, 2023 inasema kuwa Mtega amepata ajali ya kugongwa na Trekta (Power Tiller) shambani kwake Mbarali.
Spika wa Bunge, Tulia Ackson katika taarifa yake amesema “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mh. Mtega, natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, waheshimiwa wabunge na wananchi wa jimbo la Mbarali.
“Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.” Amesema Spika Tulia.
Amesema, ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.